Jumatano, 20 Desemba 2017

TAARIFA KWA UMMA,MKUTANO WA ARIMO 2018





TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA ARIMO MWEZI MACHI 2018
(ARIMO AGM)

Umoja wa wataalam wa Ardhi waliowahi kusoma Chuo cha Ardhi Morogoro unategemea kufanya Mkutano Mkuu wa mwaka 2017.Lengo la Mkutamo huu ni mwendelezo wa mikutano ya umoja huo inayofanyika kila mwisho wa mwaka ili kufanya tathimini na kujadili maendeleo ya umoja tajwa.

Viongozi wa umoja huo kwa kushirikiana na Uongozi wa Chuo unapenda kuwatangazia wanachama wake wote kwamba, Kutakuwa na Mkutano Mkuu utakaofanyika mwezi machi, 2018 katika viwanja vya chuo cha Ardhi mkoani Morogoro. Walengwa wa Mkutano huo ni watalamu wa Ardhi wote walio wahi kusoma chuo cha Ardhi Morogoro.

Aidha, Katika Mkutano huo Mgeni rasmi anatarijiwa kuwa Mh: Wiliam Lukuvi Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.Hivyo Pindi unaposikia taarifa hii mtaarufu na mwenzako.

Ardhi ni msingi Mkuu wa kufikia azma ya Tanzania ya Viwanda.

imetolewa na

Salum I. H
M/Kiti Umoja wa wataalam wa Ardhi Waliosaoma Chuo cha Ardhi Morogoro.

Kwa maelezo zaidi na mawasiliano:-
0717351395
0755040503
0713054671

posted from Bloggeroid

Maoni 2 :

  1. Tunashukuru kwa taarifa muhimu .tunaamini kwakushirikiana tutafikia malengo

    JibuFuta
  2. Panapo hitajika msaada wa fikra au mengineyo vijana wenu tupo@m/kiti salum

    JibuFuta