viongozi wa Bunge la jamii wakiwa katika viwanja vya Bunge la jamuhuri mwezi wa tisa mjini Dodoma. Picha na Deus Lugaila
Baada ya kuwa kimya kwa muda wa siku nne sasa kupisha uchaguzi wa ndani ya chama,Hatimae Bunge jamii limeanza rasm vikao vyake leo vilivyokuwa vikiendelea jijini Daresalam na katika mitandao Mbalimbali ya Kijamii.
Katika kikao chao cha leo kilichokuwa kimejikita katika kuwajadili wanawake katika ushiriki wao katika chaguzi mbalimbali za ngazi tofauti tofauti wilaya,Mkoa hadi Taifa huku kikiwasisitiza wanawake kuwa jasiri katika kuomba nafasi za uongozi katika chaguzi mbalimbali.
Akifungua kikao hicho mbele ya halaiki ya wajumbe wa Bunge jamii Leo majira ya saa nne na robo jijini Daresalam,M/Kiti wa Bunge jamii Jane Mwaswala alitoa pongezi za dhati kwa Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Magufuli Kuchaguliwa tena kwa kishindo kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na kupita bila kupingwa,aidha Mwenyekiti huyo wa Bunge jamii aliwashikuru pia wana Bunge jamii waliopata nafasi ya kushiri katika mkutano huo na kuwatia moyo kwa pongezi mbalimbali,Sanjari na hilo Mwaswala aliwashukuru kwa dhati kubwa kabisa walezi wakuu wa Bunge jamii huku akiwashukuru watanzania wote wanaoiunga mkono Bunge jamii katika kuelekea Tanzania ya Viwanda na uchumi wa Kati.
Katika hali ya kujadili hoja iliyoletwa mezani kama maada huku ikitolewa ufafanuzi yakinifu na Mwenyekiti Mwaswala aliyekuwa akiongoza kikao hicho,wajumbe mbalimbali waliwaomba wanawake kuwa majasiri na kuthubutu kuwania nafasi za uongozi katika nyazifa mbalimbali nchini.
Aidha Bunge la jamii,limewataka wanawake wote waige mifano kwa wanawake wenzao kwa kujitoa kuwania nafasi za juu za uongozi na hatimae kufanikiwa ,Akidadavua kwa mifano Mwakilishi wa Bunge jamii kutoja Mbeya Mh Shoka Alitoa mifano kwa Mh Ritta Kabati,Ummy Mwalim,Mama Sami no,na kuwaomba watanzania na jamii kwa ujumla kuiga mifano hiyo iliyohai na mifano mbalimbali.
Katika mhitasari uliotolewa na Mwenyekiti wa Bunge jamii kabla hoja kutoka kwa wajumbe kuluhusiwa ni kuwa,"Licha ya kuwa wanawake ndio sehemu kubwa ya idadi ya watu,Nguvu kazi na wapiga kura kwenye nchi nyingi za Africa,lakini ushiriki wao kwenye vyombo vya maamuzi,kuanzia ngazi ya kitaifa,Mkoa,Wilaya hadi mashina ni ndogo na haiendani na uwiano wao kwenye idadi ya jumla ya watu"
Licha ya wanachama mbalimbali wa Bunge jamii kukiri kuwa moja ya sababu sababishi ni mfumo dume,lakini bado wanombwa kujitokeza katika chaguzi mbalimbali.
Akihairisha kikao hicho,Mh Mwenyekiti wa Taasisi ya Bunge jamii inayofanya vema sasa sambamba na serikali ,Mh Mwenyekiti aliwashukuru wanachama wote na viongozi na wajumbe wa Bunge jamii na kutoa udhuru wa kutokuwepo kwa Katibu Mkuu wa Bunge jamii katika kikao kulingana na kuwa nje kwa kazi na majukumu mbalimbali ya Bunge jamii.

posted from Bloggeroid
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni