Jumamosi, 30 Desemba 2017

Bunge la jamii Tanzania,laendelea kutafasrika vyema kwa umma wa watanzania

Mlezi wa Bunge la jamii Tanzania,Mh Anthony Mavunde
Kaimu Mlezi Bunge la jamii,Mama Ritta Kabati
Katibu Mkuu Bunge la jamii Tz, Mh Rajabu Jumanne
M/Kiti,Bunge la Jamii Tz,Mh Jane Mwaswala
Wajumbe Mkutano Mkuu,Bunge la jamii,Mh Batul Kisaya na Athumany Hotty
Msemaji wa Bunge la jamii Mh Deus Lugaila.



Bunge la jamii Tanzania ni taasisi au chombo cha kijamii kinachofanya kazi kwa ukaribu na Serikali ya kuibua changamoto na kero mbalimbali zilizopo Kwenye jamii mbalimbali za kitanzania kuanzia ngazi Ya chini kabisa ya eneo la kiutawala ya Shina mpaka ngazi ya kitaifa na kuziwasilisha hizo changamoto na kero kwa mamlaka husika ikiwemo serikalini kwa ajili ya utatuzi

Bunge la jamii Tanzania ni chama cha kijamii kilichopo chini ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi kijihusishacho na masuala ya kijamii kuisaidia Serikali kufichua kero sugu na changamoto zilizofichika na si rahisi Serikali kuzifikia au kuzipata kwa haraka

Bunge la jamii Tanzania linashirikiana vyema na viongozi wa serikali wa mitaa,madiwani,wabunge,wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa,mawaziri na kila mamlaka za utawala zilizopo Kwenye nchi hii.

Bunge la jamii Tanzania ni chombo cha kujitolea kama wakala wa serikali kwa wananchi,lengo ni kuunga jitihada na ndoto za Mh Rais za kuipeleka Tanzania Kwenye uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda

Bunge la jamii Tanzania ndiyo chombo sahihi kitumikacho kuwaelimisha watanzania juu ya uzalendo wa nchi yetu,kuifahamu Serikali yao,nchi,rasilimali za nchi na kuuhimiza umma wa watanzania kufanya kazi kwa bidii

Bunge la jamii Tanzania ni chombo kitumikacho kupinga kwa nguvu zote vitendo vyote visivyo vya kimaadili ya kitanzania,madawa ya kulevya,uvutaji bangi,unyanyasaji wa kijinsia,ukeketaji,mauaji albino,vikongwe na ongezeko la watoto wa mitaani kwa ustawi wa nchi yetu.

Bunge la jamii Tanzania ni chombo ambacho ni Sauti ya wanyonge ya kufikisha mawazo,maoni na kero za watanzania kwa haraka kwa mamlaka husika kwa utatuzi na ustawi wa jamii za kitanzania ikiwemo kulinda na kutunza utamaduni wa kitanzania na kudumisha amani ya nchi




Like na share page rasm ya Bunge la jamii tz

posted from Bloggeroid

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni