Ijumaa, 29 Desemba 2017

Funga Mwaka,Bunge la jamii kufanya ziara Hospital ya wilaya ya korogwe na kutoa misaada kwa wagonjwa

Funga Mwaka,Bunge la jamii kufanya ziara Hospital ya wilaya ya korogwe na kutoa misaada kwa wagonjwa


Baadhi ya wanachama wa Bunge jamii wakiwa katika sherehe ya uzinduzi wa Bunge jamii mjini Dodoma



Katika kufunga mwaka na kuanza mwaka mpya,Bunge la jamii Tanzania kupitia mkoa wa Tanga linatarajia kufanya ziara katika hospital ya wilaya ya Korogwe ijulikanayo kama Magunga kwa ajili ya kutoa misaada kwa wagonjwa mbalimbali na kusikiliza kero zao mbalimbali na Changamoto kwa makundi mbalimbali yawagonjwa na kuzifikisha kwa mamlaka husika.

Sanjari na hilo Bunge la jamii litayahudumia makundi mbalimbali kama watoto yatima ambapo pia litapata fursa ya kuonana na uongozi wa kituo cha yatima mkoani Tanga.

Taratibu zote za kuonana na uongozi wa hospital itakayoenda kutembelewa na wanachama wa Bunge la jamii Tanga,tayar umeshafanyika na mipangilio inaenda vizuri.

Ikumbukwe kuwa Taasisi ya Bunge la jamii niyawatanzania wote yaani wananchi kwa ujumla ikiwa na lengo la kuibua kero,Changamoto mbalimbali kuzifikisha kwa mamlaka husika sanjari na kuunga mkono kazi ya Mh Rais na adhima yake njema ya Tanzania ya Viwanda na uchumi wa Kati .





Msemaji wa Bunge la jamii Tanzania
Deus Lugaila
0765392196

posted from Bloggeroid

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni