Zikiwa ni siku chache toka mkuu wa mkoa wa Morogoro kupata ajari akitokea katika utekelezaji wa majukum ya kitaifa,Bunge la jamii Tanzania kushirikiana na chama cha mapinduzi tawi la jordani wametuma wawakilishi kumtia moyo na kumpa pole Mkuu huyo kufuatia ajiri hiyo aliyoipata siku chache nyuma.
Mbele ya Mkuu huyo wa mkoa, wawakilishi hao walimuhakikishia kuwa Bunge la jamii lipo kwa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na hilo huku wakimuhakikishia kuwa wataendelea kuibua kero mbalimbali kama wanavyoendelea kwa kupatiwa ufumbuzi zaidi.
Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa kwa uchungu uliojaa furaha aliongea maneno ya kuwashukuru wanabunge jamii na ccm kwa hisia kali huku akiwahakikishia kuwa yupo upande wao.
Sanjari na hilo ,Mkuu huyo amelisifia Bunge la jamii Tanzania na viongozi wake kwa uwajibikaji wao kuhakikisha wanaibua kero kama wanavyoendelea kufanya na kuwadhihirishia kuwa pamoja nao hata katika kongamano la Bunge la jamii mkoa wa Morogoro kuwa atahakikishia analisimamia ipasavyo kumuunga mkono Mh Rais na amesema kuwa nia ya Bunge la jamii Tanzania ni njema sana hususani kwa awamu hii ya Tano inayofanya vizuri kuelekea Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati,
Baada ya salam kwa mkuu huyo wa mkoa,wanachama wa Bunge jamii na wanachama wa ccm walipata fursa ya kupiga picha na mkuu huyo na viongozi mbalimbali ofsn kwake huku wakiliombea taifa amani na kumuombea mh Rais na viongozi wake
Na
Deus Lugaila
Msemaji na Mratibu Bunge la jamii Tanzania
posted from Bloggeroid
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni