Bunge la jamii Tanzania linalofanya vizuri sasa huku likishirikiana na wadau mbalimbali wenye mapenzi mema ya Nchi yao hususani kumuunga mkono Mh Rais katika adhima yake njema ya kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa kati na yenye viwanda ikishirikiana na chama cha mapinduzi kwa ukaribu zaidi,limejipanga kufunga mwaka kwa tukio la kihistoria na kuja kivingine kwa mwaka 2018 .
Wakiongea na mtandao wa Bunge jamii,viongozi wa Bunge jamii Taifa wamesema watakuwa na hafla ya kufunga mwaka ya Bunge la jamii itakayofanyikia mkoani Morogoro tarehe 9,12,2017 kama tarehe hiyo haitabadilika.
Akidhibitisha kuwepo kwa hafla hiyo ambayo ni kongamano la vijana huku kukiambatana na uzinduzi wa Bunge jamii mkoa wa Morogoro,Katibu wa Mkoa wa Morogoro Mh Dan Ford amesema hafla hiyo ipo na maandalizi yanaendelea vizuri huku akiwakaribisha watanzania wote.
Hafla hiyo pia itaambatana na kugawa kadi za uanachama wa CCM na Bunge jamii Tanzania huku ikiuzuliwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa.
Akiongea kwa njia ya simu,Msemaji kiongozi wa Bunge la jamii Taifa,amewataka watanzania wote wenye mpenzi mema na nchi yao Kuhudhuria hafla hiyo yenye nia njema na taifa huku ikiwatunuku wanachama wa chama cha Mapinduzi kadi za uanachama na kuwapokea wanachama wapya wa Bunge jamii.
Sanjari na hilo,naye Katibu mkuu wa Taasisi ya Bunge jamii akiwa na Mwenyekiti wake kwa njia ya simu akiongea na mtandao wa Bunge jamii alidhibitisha kuwa uwepo wa hafla hiyo ya funga mwaka inatarajia kufanyika Morogoro huku wakidhibisha uwepo wao katika hafla hiyo,wamesema kuwa wameona wafunge mwaka na tukio la kijamii na kitaifa nchini.
Nae mlezi msaidizi wa Bunge la jamii Tanzania,Mh. Ritta Kabati amebariki hafla hiyo kama itafanikiwa kufanyika tarehe hiyo na kuomba radhi kutoshiriki kutokana na kuwa Daresalaam katika halakati za kitaifa.
Viongozi wa kitaifa wa Bunge la jamii wanaotarajia kufika katika hafla hiyo nipamoja na Mwenyekiti wa Bunge la jamii Tanzania, Katibu Mkuu Kiongozi Bunge la jamii,Msemaji Kiongozi Bunge la jamii,Kaimu Katibu na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Bunge la jamii,na viongozi mbalimbali wa kitaifa wa kiserikali wa Bunge la jamii Na viongozi mbalimbali nchini.
Uwepo wa Tukio hilo umepokelewa vyema na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Kabwe na kuungwa mkono na Taasisi mbalimbali zilizopo mkoani humo.
Hafla hiyo inatarajia kufanyika siku ya jumamosi kama haitabadilishwa tarehe zake.
posted from Bloggeroid
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni