Jumapili, 24 Desemba 2017

FRIENDS OF BATULI INAWATAKIA WATANZANIA WOTE SHEREHE NJEMA YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA





Taasisi ya Friends of Batul kupitia kwa msemaji wake kiongozi Mh Batul Kisaya ametoa salamu za kheri za Taasisi hiyo kwa watanzania huku akiwawasilisha viongozi wa Taasisi hiyo.

Akiongea na mtandao wa BJT kwa njia ya simu,Msemaji huyo wa Friends of Batuli alimesema kuwa Friends of Batul imeweza kufanya mambo mbalimbali ndani ya mwaka huu na mpaka muda huu imefanya harakati mbalimbali nchini hususani kwa mkoa wa Arusha.

Akiwashukuru watanzania wote kwa niaba ya taasisi hiyo,msemaji huyo amesema kabla ya kufunga mwaka friends of Batul wanatarajia kufanya hafla fupi kwa vikundi vyenye uitaji,kama yatima nk.hata hivyo msemaji huyo ameshindwa kuweka wazi mipango yao ya mwakani na kusema kuwa ratiba hiyo itatoka hapo baadae na baada ya mwaka mpya.

Msemaji huyo wa Friends of Batili amewasihi watanzania kuwa watulivu katika kipindi hiki cha sikukuu na kuwaomba wasivunje sheria zozote zile za Nchi na kuwasihi washerekee salama salimin.

Friends of Batuli ni Taasisi inayojishughurisha na kusaidia jamii zenye uitaji kama yatima,wajane na jamii mbalimbali zifananazo na hizo

posted from Bloggeroid

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni