Habarini wana wa Mungu.
Ni siku kadhaa toka vikao vya Bunge la jamii visimamishwe kwa ajili ya kupisha zoezi la uzinduzi wa taasisi hiyo.
Tunamshukuru Mungu tumemaliza salama swala la uzinduzi,kujipambanua kwa watanzania na kwa serikali.
Tunawashukuru wote walioweza kufanikisha shughuri hiyo na hata ambao hawakupata nafasi ya kushiriki si mbaya watashiriki hata kwa kazi nyingine ya kitaasisi.
Mama Ritta Kabati,Mama Faida Mohamedi,Mh Stanislaus Mabula,Mh Mavunde,makatibu mbalimbali wa mawaziri na wabunge mbalimbali wa jamhuri ikiwa ni pamoja na viongozi wa kiserikali,na wanachama wote tunawashukuru kwa ufanikishaji wenu na uwepo wenu siku ile ya shughuri kwa mantiki hiyo,nasema Mungu awabariki sana.
Kuanzia kesho jumatatu tutaendelea na mijadala ya maada kama ilivyokawaida yetu ya uibuaji kero changamoto mbalimbali na kuzifanyia upembuzi wa kina na waheshimiwa wabunge kuzifanyia kazi.
Endelea kufuatilia ukrasa huu ili upate kujua baada ya uzinduzi wa Bunge la jamii nini kinafuata .
Uongozi unatarajia kuweka muda wowote mambo ya kufanya sasa baada ya uzinduzi,huku unatarajia kuboresha kila sekta na kutembelea kila mkoa.
Na
Deus Lugaila
Msemaji Bunge la jamii
posted from Bloggeroid
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni