Bunge la jamii limefanya uzinduzi wake mapema hapo Jana huku mgeni rasm akiwa Mh Anthony Mavunde Naibu Waziri ambae aliwakilishwa na Mh Mabula Mbunge wa Nyamagana Mwanza.
Hafla hiyo iliyovitikisa hata vyombo vya habari nchini iliambatana na utoaji tuzo za vyeti vya pongezi kwa wanachama na viongozi mbalimbali nchini.
Pamoja na viongozi waliotunukiwa vyeti ni,Mh Jobu Ndungai,Mh Anthony Mavunde,Rita Kabati, na wanachama ni pamoja na Esther Shoka,Richard Nnko,Damian Semba,Dickson Lubui,Barut CharlesMoris makalius na Friends of Batuli .Hao wote walipewa cheti vya pongezi kwa kuiwasilisha jamii vyema ya kitanzania.
Wakiongea kwa nyanja tofautitofauti,wale wote waliotunukiwa tuzo hizo waliwashukuru watanzania kwa kulipokea vyema Bunge la jamii ambalo limekuja mahususi kufanya kazi za kijamii nchini.
Bunge la jamii limekuja na mtazamo chanya kwa watanzania Mara tu baada ya Risala kusomwa na hotuba ya mgeni Rasm.
Watanzania mbalimbali nchini wamelipongeza Bunge hilo la jamii kwa kazi hiyo ya kijamii.
posted from Bloggeroid
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni