Jumanne, 12 Septemba 2017

RITA KABATI MBUNGE,ANENA MAZITO KWENYE UZINDUZI WA BUNGE LA JAMII,AWAOMBA WABUNGE WOTE KUTOA USHIRIKIANO KWA TAASISI HIYO







Ikiwa ni siku kazaa sasa zimepita,wanachama wa taasisi ya Bunge la jamii kufanya uzinduzi wao mjini Dodoma huku wabunge mbalimbali wakihudhuria hafla hiyo.

Mbunge wa Viti Maalum kutoka Iringa ambae pia ni mlezi msaidizi wa Bunge la jamii Tanzania,alinena maswala mazito katika uzinduzi huo na kuwaomba wabunge wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kushirikiana vema na Bunge jamii katika kuhakikisha wanatatua changamoto mbalimbali katika jamii na kumuunga mkono Mh Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania katika kuindea Tanzania ya uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda.

Mh Rita Kabati alienda Mbali zaid na kusema,hoja nyingi atoazo Bungeni ni kutoka kwa Bunge jamii,kwani ni mdau Mkuu wa Bunge jamii,amesema ujio wa Bunge la jamii,utawasaidia hata wao katika majimbo yao kutatua na kuibua kero katika jamii kwa maendeleo ya taifa.

Akihutubia kwa muda mfupi baada ya kupewa nafasi ya kuongea,Mh Faida Bakari mbunge kutoka Pemba,akihutubia katika uzinduzi huo aliwaomba wanachama wa Bunge la jamii kufika Pemba ili kufanya kazi za kuibua kero ,changamoto mbalimbali katika jamii kwa maendeleo ya taifa.

Bunge la jamii,imekuwa taasisi ya kwanza itokanayo na mitandao ya kijamii kufanya kazi na serikali kwa nyanja Mbali Mbali nchini.

posted from Bloggeroid

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni