Naibu Waziri vijana ajira na wenye ulemavu Mh Anthony Mavunde, anatarajia kuzindua Bunge la jamii kwa maendeleo ya taifa siku ya jumamos tarehe 9/9/17,Katika ukumbi wa Veta uliopo katika chuo cha Veta mjini Dodoma, huku ukiuzuriwa na viongozi mbalimbali nchini.
Uratibishaji wa uzinduzi huo unaendelea kuratibishwa na viongozi wa taasisi hiyo kwa ufanisi zaidi.
Viongozi mbalimbali wa kiserikali wakiwemo na wabunge wa jamhuri ya muungano wa Tanzania wamealikwa katika uzinduzi huo mjini Dodoma.
Bunge la jamii ni mfumo upya unaoingia nchini kwa Mara ya Kwanza kabisa hasa kuja kushirikiana na serikali kwa mambo mbalimbali ya kijamii,kiutamaduni, kielimu na kiuchumi.
Aidha mfumo huu waweza kuigwa na Nchi za jirani hata Africa kwa ujumla kutokana na utendaji kazi wake.
posted from Bloggeroid
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni