Jumamosi, 25 Novemba 2017

WADAU WA BUNGE LA JAMII MOROGORO WAMWANDIKIA WARAKA RC KABWE,USAILI WA JKT






CHANGAMOTO KWA VIJANA WALIOPATA NAFASI YA KUINGIA KATIKA NGAZI YA USAILI WA KUJIUNGA NA JKT MKOA WA MOROGORO KUTOKA WILAYA MBALIMBALI ZA MKOA.


Mhe. Mkuu wa Mkoa tumekutana na changamoto kutoka kwa baadhi ya vijana wa Mkoa wetu ambao wako hapa kwaajili y usaili wa kujiunga na JKT ambapo kutokana na kujitolea wamekuwa wakikaa katika nyumba za kulala wageni na kujitegemea chakula tangu Tarehe 16/11/2017
Mpaka sasa bado taratibu zinaendelea lakini wameambiwa kusubiri hatua ya vipimo.

Sisi ni vijana tulioko mkoani morogoro kwa ajili ya usaili wa jeshi la kujenga taifa(jkt) tunaowakilisha wilaya mbalimbali ambapo kwa sasa tupo mkoani na tunaendelea vizuri,ila tunakabiliwa na changamoto ambazo ziko juu ya uwezo wetu kama CHAKULA na KODI ya mahala tunapokaa, tumejalibu kusaidiana sisi kwa sisi kama kuchangiana chakula na kodi lakini bado tunakwama kulingana na hali zetu especial watoto wa kike hali zao sio nzuri kabisa .kwa umoja wetu tunawaomba ndugu zetu mtusaidie.

NIMANENO YA MMOJA WA VIJANA AKIELEZA
Mhe. Mkuu wa Mkoa na pia Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama
Vijana wako wa Bunge la Jamii Mkoa wa Moro team yako ya kazi Tunaomba sana utusaidie vijana wenzetu zoezi lao liende kwa haraka kiasi ili walau warudi majumbani siku si nyingi au VILE UTAKAVYOONA INAPENDEZA BABA YETU
AHSANTE SANA



© wadau wa Bunge la jamii

posted from Bloggeroid

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni