Toleo la 7 la Tarehe 23/11'2017
Mwendelezo wa makala za harakati za kimapinduzi Ya kifikra
KANUNI ZA KIMAISHA ZITAKAZOKUFANYA UFIKIE MAFANIKIO YAKO YA KIMAISHA
Natumaini kuwa wasomaji wangu na watu wote wanaofutilia masomo haya kwa njia mbalimbali za kimitandao huko mliko hamjambo,mungu awabariki sana.
Kama ilivyo desturi yangu kuwa huwa naandaa na kurusha mitandaoni masomo haya usiku kwenye facebook na asubuhi kwenye blogs na groups Za whatsapp,leo narusha masomo haya nikiwa mjini magu hapa na kesho saa nne asubuhi ntakuwa nimewasili mjini mwanza mtaa wa California Kata Ya Nyegezi.
Naanzia ñilipoishia somo lililopita kwenye kanuni hii Ya kubana matumizi katika kipengele cha njia Ya kujilazimisha kubana matumizi ambayo ni Kupunguza mahitaji yote yasiyokuwa Ya lazima na yakikosekana hayawezi kuathiri maisha yako.
Leo naendelea na kanuni hii na ninaihitimisha kwenye kipengele hiki ambacho ni cha mwisho kwenye kanuni hii,kinaitwa *kuepuka kuhemea mahitaji Ya rejareja,jizoeze kuhemea mahitaji Ya jumlajumla*huenda haya maneno yasieleweke kwa haraka na kwa wepesi,lugha rahisi mahitaji Ya rejareja ni yale mtu ananunua kila siku kama ni mchele kwake wanakulaga kilo mbili kila siku ananunua kilo mbili hizo dukani,kama anapikiaga fanta moja ya mafuta Ya kula kila siku ananunua fanta moja dukani,kama ni mkaa wa Tsh elfu 1000 kila siku atanunua kijiweni mkaa wa elfu 1000,kama ni vitunguu na nyanya za Tsh elfu 1000 kila siku atanunua vitunguu na nyanya za elfu 1000,haya ndiyo mahitaji Ya rejareja.
Lakini mahitaji Ya jumla ni mahitaji ambayo mtu anunua vitu vingi kwa pamoja vya kutumia muda mrefu,matharani kama ni mchele hanunui kwa kilo bali mfuko mzima au gunia ,unga mfuko mzima,mkaa atanunua gunia,mafuta Ya kupikia dumu la lita 5 au10 n. K Kama ni nyanya au vitunguu ni tenga au kindoo cha vitunguu,haya ndiyo mahemezi Ya jumla jumla.
Tunafanya haya yote ili kutafuta unafuu wa maisha ili tufanikishe na mambo mengine Ya kimaisha isiwe siku zote wewe mafanikio yako ni hela Ya kula tu ila hela Ya kujenga na kuanzisha biashara huioni,sio kwamba haipo ipo lakini imemezwa na haya matumizi ukidhibiti matumizi kwa uaminifu utaiona hela yako inakuambia yenyewe kuwa ipo hapa ukaiweke akiba.
Ninahakika kwa watu ambao hawatachukulia mzaha masomo haya kwa maana Ya vitu vya mitandaoni tu havina maana yoyote vya watu waliokoswa kazi basi utabaki vilevile maana ukiugua kanuni Ya kupona ni kunywa dawa lakini kama hutaki dawa unataka ugonjwa ukuue,kwa wale ambao watafanyia kazi kwa uaminifu hata tusipoonana leo tutakujaga onana mtatoa ushuhuda.
Kuna Shida kubwa sana kwenye kona hii ya matumizi Ya reja reja kwa kuwa unanunua kwa hela kubwa na vinaisha siku hiyo hiyo kwa kuwa unaitoa hela uliyoitafuta siku hiyo au uliyo nayo mfukoni siku hiyo utaiona ndogo ila ukitaka kuijua kuwa ni kubwa kiasi gani andika tu kila siku mwisho wa mwezi jumlisha uone ni kiasi gani cha pesa kilichotumika kwenye hicho kitu.
Matharani familia yako huwa wanakula kilo mbili za unga mlo wa mchana,kila mchana ukitaka kusonga ugali unaenda kwa mangi au kwa muha akupe unga kilo mbili,kila kilo Tufanye elfu 1000 bila kujali dona au sembe,kilo mbili ni elfu 2000 siku moja kwa mwezi siku 30 ni elfu 60000,huu ni unga,kwa sasa debe la mahindi lina elfu 12000 kwa nini usinunue mahindi debe mbili kwa gharama ya elfu 24000 tu, ukisaga na kukoboa tufanye iwe elfu 27000 kwenye elfu 60000 inabaki elfu 33000,hapa umesaga unga wa kula zaidi Ya mwezi na umeokoa hiyo hela.
Mafuta Ya kupikia kila siku unatoa elfu 1000 hesabu Ya kawaida kabisa kwa mwezi ni elfu 30000,kwa nini usinunue dumu la lita 5 kwa elf 17000 ukaokoa elfu 13000 na mafuta ukatumia zaidi Ya mwezi,masomo haya wengi watasema tunajifunza uchoyo na ubahili,lakini ukweli tunajifunza strategies za maisha ili maisha yawe mepesi.
Mkaa kila siku unatoa elfu 1000 kwa mwezi ni elfu 30000 kwa nini usinunue gunia la mkaa elfu 45000 ukatumia miezi 3 kuliko elfu 30000 mwezi mmoja na miezi 3 ni elfu 90000 hapa utakuwa umeokoa elfu 45000.
Angalia Mchele kwa hesabu hizo hizo za kilo mbili kwenye familia yako kila siku kwa sasa mchele dukani kilo moja ni elfu 2000 kilo mbili ni elfu 4000 kwa mwezi ni laki 120000,kwa nini usinunue gunia kwa Tsh elfu 90000 ukalikoboa na utalitumia kwako zaidi Ya mwezi mmoja na ukawa umeokoa elfu 30000.
Hii ni mifano tu lakini hakikisha kila hitaji lako unaanza kujizoeza kufanya mahemezi Ya mahitaji yako Ya mwezi mzima ili kuokoa pesa kutumika nyingi,mahitaji Ya rejareja yanatumia hela kubwa sana ukija ukajumlisha kwa mwezi utapata umetumia gharama kubwa tofauti na mahemezi Ya mwezi mzima.
Usipofikia hatua ukakisumbua kichwa kuyabaini haya na ukaamua kudhibiti matumizi huenda ukatapatapa sana kimaisha mwisho wa siku utakutwa na uzee ukaanza kulaani bure hata wanao kuwa hawakujali kumbe ungetafutaga vyako ingali una nguvu uzee ungekukuta una akiba za kutosha.
Maisha ni kanuni ukikosea kanuni hutapata jibu sahihi,naishia hapa leo kesho naendelea na kanuni nyingine ya kimaisha,kazi yako nikunifuatilia mpaka ntakapohitimisha masomo haya yote,usiache kulike,kucomnent na kushare na nifuate facebook kwa kutuma ombi la urafiki ili uendelee kufuatilia mtiririko wa masomo haya yote.
Maoni yako 0717523952
Na mchambuzi wetu
Julius Mabula
posted from Bloggeroid