Ijumaa, 4 Mei 2018

KIONGOZI WA BUNGE JAMII ATEULIWA NA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA

Deus Lugaila,Msemaji Bunge jamii






Mseaji na Kiongozi wa juu wa Taasisi ya Bunge la jamii ambayo imefanya vizuri sana katika kipindi cha siku za hivi karibuni ambayo kwa sasa imesimama ili kukamilisha masuala ya kisheria, Mh Deus Lugaila Ameulamba mkwanja kwa kuteuliwa na chama cha Shule za Binafisi Tanzania kuwa afisa habari na Msemaji wa Chama hicho Nchini.

Akipiga story na Mwanahabari wa Blog ya Greave,Mara baada ya mwanahabari huyo kuomba kujua kama ameupokea huo wito,Mr Lugaila alisema "Nimepokea barua ya uteuzi kama Afisa Habari ngazi ya Taifa ndani ya chama,nitashirikiana nao bega kwa bega katika harakati za kulipeleka Taifa katika uchumi wa kati na Taifa lenye viwanda na wasomi wengi Alisema Mr Deus huku akiongeza kuwa kuteuliwa kwangu kama Afisa habari ndani ya chama hicho hakiathiri chochote katika nafasi yangu ya Bunge jamii.alisema kiongozi huyo.

Ikumbukwe kuwa Deus Lugaila ni kiongozi wa Bunge jamii ambalo kwa sasa limesimama kiutendaji katika harakati za kukamilisha masuala ya kisheria,kiongozi huyo amejizolea umaarufu katika kipindi kifupi kutokana na misimamo yake ya kujenga hoja huku akilitangaza Bunge jamii vyema kwa umma na kuuhamasisha umma kuendana na Sera ya Mfumo wa Taifa sanjari na Kuunga Mkono Serikali ya awamu ya Tano.

posted from Bloggeroid

Jumatano, 31 Januari 2018

Maandalizi ya Uzinduzi Bunge jamii Morogoro

Maandalizi ya shughuli ya kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya Tano sanjari na kuzindua Bunge jamii Mkoa wa Morogoro unaendelea kufanyika